SGR Tanzania

SRG ni nini?

SRG ni ufupisho wa neno la kiingereza “Standard Gauge Railway”.
Ni reli ya kisasa yenye upana wa mita 1.435, na inayopatikana duniani kote kwa zaidi ya asilimia hamsini na tano (55%).
Tofauti na reli ya kawaida, reli hii inUweza kusafirisha uzito mkubwa na kusafiri kwa mwendo kasi.

 

TANZANIA NA SGR

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia shirika la reli Tanzania (TRC) imeazimia kujenga reli hii ya kisasa kueneza mtandao usiopungua km 2,561 ikiunganisha mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza, Kigoma, Katavi na nchi zinazokuwa na bandari (Rwanda, Burundi, DRC).
SGR ni reli ya kisasa na ya kwanza Africa mashariki na kati itakayokuwa na uwezo wa kupitisha treni zitakazoendeshwa kwa nishati ya umeme na yenye mwendo kasi usiopungua kilometa 160 kwa saa.
Lengo la reli hii ni kuongeza ufanisi katika sekta ya usafirishaji nchini ususani sekta ya reli ambapo yafuatayo yatarahisishwa;
Ongezeko la usafirishaji wa mizigo ambapo reli itabeba mzigo wa mpaka tani 10,000 kwa mkupuo sawa na uwezo wa maroli 500 ya mizigo.
Uokoaji wa muda kwa usafiri wa abiria na mizigo ambapo itasaidia kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla. Ongezeko la ajira kwa wazawa katika sekta na fani mbalimbali.
Oboreshaji wa huduma za kijamii ikihusisha ujenzi wa shule, vituo vya afya na ujenzi wa barabara katika maeneo yanayo pitiwa na mradi.
Kuchochea maendeleo katika secta ya kilimo, biashara, madini na viwanda hususani katika maeneo ambapo reli hiyo inapita pamoja na kwa nchi jirani hasa Rwanda, Burundi, Uganda, Kenya na DRC.
Faida za kiuchumi kwenye sekta ya usafirishaji hasa kupunguza gharama za mara kwa mara za matengenezo ya barabara. Ujenzi wa reli ya kisasa kwa nchi yetu wenye mtandao wa km 1,219 za njia kuu, upo katika awamu tano na ni kama ifuatavyo;

• Awamu ya 1 Dae es Salaam – Morogoro (Km 300)
• Awamu ta 2 Morogoro- Makutupora (Km 422)
• Awam ya 3 Makutupora –Tabora (Km 294)
• Awamu ya 4 Tabora – Isaka (Km 130)
• Awamu ya 5 Isaka – Mwanza ( Km 249)

 

MUUNDO NA MPANGILIO WA RELI YA KISASA (SGR)

Reli hii ya kisasa inajengwa sambamba na reli iliyopo (MGR) isipokuwa maeneo maeneo machache yenye kona kali. Ujenzi wa reli hii unazingatia uhifadhi wa mazingira na usalama wa watu na mali zao.

• Sehemu za mwingiliano wa magali na reli, kutakuwa na aidha kivuko cha juu na chini.
• Uzio unajengwa kwa usalama wa watu na wanyama.
• Elimu kuhusiana na usalama kwa ujumla itatolewa mara kwa mara.

 

Nafasi za kazi

Mradi wa SGR Tanzania unatoa fursa za ajira za muda mfupi zaidi ya 30,000 katika fani mbalimbali kwa wananchi ambao wanakidhi vigezo vifuatavyo :-

  • Uwe na umri wa miaka 18 au zaidi.

  • Uwe na elimu ya kidato cha nne au zaidi mwenye kujua kusoma na kuandika kwa ufasaha.

  • Uwe mwenye afya njema na akili timamu.

  • Uwe na kitambulisho cha taifa

  • Uwe tayari kufanya kazi katika mazingira tofauti sawasawa na atakavyopangiwa.

Malipo ya ajira ya muda mfupi

Mgawanyiko wa malipo kwa siku ni kati ya 70,000 - 150000 kutokana na sifa za muajiriwa. Muajiri atawajibika na malazi pamoja na usafiri katika eneo la kazi

    ZINGATIA

  • Malipo yote yatafanyika kupitia account ya bank ya muajiriwa.

 

 

Hitimisho

Ujenzi wa barabara za lami, meli katika ziwa Victoria, reli ya kisasa (SGR) na uboreshaji wa viwanja vwa ndege ni dhamira ya Serikali kuunganisha mikoa na nchi jirani kwa usafiri wa njia zote hivyo ni vema kwa watanzania kujivunia miradi hiyo na kuonesha uzalendo kwa kuitunza. Serikali inatambua umuhimu na manufaa ya kugawa fursa pindi zinapojitokeza moja kwa moja kwa wananchi wake kwani ndio walengwa wa miradi na inabidi wanufaike nayo.

 

Rejea juu

© 2023 SGR Tanzania